Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula anatumia jina langu ku-trend - Abby Chams

Abby Chams Paula(1) Paula anatumia jina langu ku-trend - Abby Chams

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Abigail Chamangwana 'Abby Chams' amesema kuwa hawezi kumzungumzia mwanadada mwenzake, Paula Kajala kwani atakuwa kama anampa ngazi ya kutembelea upepeo wake ili ku-trend mitandaoni.

Abby Chams amesema hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Alfred Bundala wa SNS kufuatia wawili hao kupishana mitandao kisa kikidaiwa kuwa ni mpenzi wa Paula, yaani Marioo kufuta verse ya Abby kwenye ngoma yake ya Love Song.

“Mimi sikuwa karibu sana na Paula lakini watu wanapenda sana ku-trend, siwezi kusema sana maana watatumia jina langu kwa ajili yak u-trend. Mimi sio mtu ambaye natumia muda mwingi mitandaoni, muda mwingi niko darasani au studio ninafanya music.

“Sikumbukumbuki nimekutana na Paula mara ngapi lakini nakumbuka alinialika kwenye birthday yake laki sijazoeana nae. Mimi nina mahusiano mazuri na wasanii karibu wote wa kike, wapo ninaozungumza nao, tunafanya kazi pamoja, tunapigiana simu na kushauriana mambo mbalimbali lakini siwezi kuwataja,” amesema Abby Chams.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live