Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula ana jambo lake kubwa Ijumaa, aibua mjadala

Paula Anapiga Hatua Paula ana jambo lake kubwa Ijumaa, aibua mjadala

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto pekee wa muigizaji Kajala Masanja, Paula ametangazwa kuwa ana jambo kubwa analokwenda kulifanya kesho kutwa Ijumaa Agosti 5, 2022.

Taarifa za ndani zinadai kuwa, Paula anakwenda kulamba dili la ubalozi wa duka kubwa mjini lakini vyanzo vingine vikieleza kuwa, anataka kuanza maisha ya kujitegemea ili aweze kutoka katika nyumba ya mama yake na baba yake wa kufikia, Harmonize.

Hata hivyo, kuelekea kwenye siku hiyo, mtandaoni mjadala mkubwa ni kwa nini jambo hilo litangazwe kupitia vyombo vya Wasafi wakati ni hasimu wa Harmonize.

Kupitia ukurasa wa Wasafi TV Instagram, wameposti bango lenye picha ya Paula na kuandika: “amekua, anapiga hatua.” Bango hilo limeonesha kuwa jambo hilo litajulikana Agosti 5, mwaka huu na litarushwa na Wasafi TV.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live