Moja kati ya habari mpya zinazotrend leo ni hii ya mtoto wa muigizaji Kajala Masanja, Paula kudaiwa amefunga ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Ally.
Gumzo zaidi limechagizwa na mama yake mzazi kumpongeza kupitia ukurasa wake wa Instagram na watu wengine kuamini kweli huwenda ikawa ni ndoa lakini wengine wakiamini ni kiki.
"Mungu akutangulie katika maisha yako haya mapya dada pau ukawe mke bora na sio bora mke???????? Mrs ALLY"
Miongoni mwa watu ambao hawakuamini ishu hiyo ni pamoja na kaka yake Diamond Platnumz, Rommy Jones ambaye amekomnti kwenye picha alizoposti Kajala na kumpongeza binti yake huyo wa pekee.
"ACHENI UONGO WASANII JAMANI."