Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula afunguka kuhusu mama yake kupokonywa Range na Harmonize

Paula Harmonize Paula, Kajala na Harmonize

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja, Paula amejibu madai ya kuwa walipokonywa gari la kifahari aina ya Range Rover na aliyekuwa mpenzi wa mama yake, Konde Boy Harmonize.

Gari hilo ambalo Harmonize alimzawadi Kajala kama ombi la kutaka kurudiana naye baada ya kutengana kwa mara ya kwanza ndilo lililokuwa likizungumziwa.

Kupitia video hiyo ambayo inatrend TikTok, ilirekodiwa na mpiga picha wa Paula, Benard Atilio ambaye ndiye aliyemuuliza iwapo madai ya kupokonywa Range hiyo yalikuwa ya kweli.

"Nasikia mmenyang'anywa Range," aliulizwa Paula na Benard Atilio. Paula alimjibu kwa kusonya tu na kucheka ila hakufafanua iwapo ni kweli wamepokonywa au ni madai tu.

Hata hivyo, jibu la Paula linashiria kuwa bado Kajala hajapokonywa gari hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live