Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula adaiwa kurudiana Rayvanny

PAULA NA RAYVANNY Paula adaiwa kurudiana Rayvanny

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paula Kajala au Pau; ni mwanamitindo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) ambaye anadaiwa kurudiana na msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny au Vanny Boy na kuendeleza penzi lao pale lilipoishia.

Miezi kadhaa iliyopita, baada ya mama mzazi wa Paula, Kajala Masanja kurudiana na msanii Harmonize ilisemekana kwamba Paula ameachana na Rayvanny kwa kuwa jamaa huyo ni hasimu mkubwa wa Harmonize.

Wachambuzi wa Insta walisema kuwa, Paula asingeweza kuendelea na Rayvanny ilihali anaishi nyumbani na kuhudumiwa kila kitu na Harmonize.

Na hilo lilithibitika baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa, hata duka alilozindua Paula hivi karibuni lina mkono wa Harmonize ambaye alihudhuria siku ya uzinduzi.

Taarifa mpya ni kwamba, Paula na Rayvanny wameonekana pamoja kwa mara nyingine huku mrembo huyo akimaliza utata kwa kusema; “Siwezi kumuacha…”

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Snapchat, Paula ameulizwa kama bado yupo na Rayvanny? Ambapo mwenyewe amejibu; “Real Bad, Siwezi muacha…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live