Mtoto wa Kajala Masanja, Paula anadaiwa kunasa ujauzito wa mpenzi wake saa wa Bongo Fleva, Marioo.
Hiyo imekuja kufuatia Marioo kumpa Paula pongezi zenye utata katika ukurasa wake wa Instagram na watu kuona mabadiliko ya muonekano wa Paula.
Waandishi wa habari walimbana maswali Paula na mama yake jana walipokuwa wanazindua duka lao jipya maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
"Omari alimpongeza Paula kwa kufungua duka na sio vinginevyo. Nadhani watu walivyoona hivyo ndio wakajiongeza, na kama akinasa mimba kwa umri wake sioni tatizo mbona vijijini watu wanabeba mimba na miaka 14?," alihoji Paula.
Kwa upande wake Paula alipoulizwa kuhusu pua yake kuonekana kuvimba, alisema si kwamba ana mimba. "Sina mimba mimi," alijibu Paula.