Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula: Zuchu ndo mshauri wangu

ZUCHU NA Paula: Zuchu ni mshauri wangu

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa hujui chukua hii kutoka hapa! Mtoto wa muigizaji Kajala Masanja, Paula ana uhusiano wa karibu sana na Zuchu, staa wa Bongo Fleva.

Paula amefunguka hayo Agosti 3, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM kuhusu jambo lake kubwa analokwenda kulifanya kesho kutwa Ijumaa.

“Zuchu ni dada kwangu ni mshauri na nilifahamiana naye muda tu, ikitokea nina jambo nataka ushauri basi huwa ananishauri lakini pia mimi nampenda, napenda muziki wake,” alisema Paula.

Kwenye mahojino hayo Paula alisema pia hana kinyongo na baba yake ambaye ni Prodyuza P Funk na anatarajia kwenda kumsalimia Arusha hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live