Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula: Nina mpenzi, sitaki kumuongelea Rayvanny

Paula Vanny Boy Paula an Rayvanny

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sosholaiti na mtoto wa muigizaji Kajala Masanja, Paula ameweka wazi kuwa anaye mpenzi na hataki kuzungumza kuhusu Rayvanny.

Paula amefunguka hayo Agosti 3, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM kuhusu jambo lake alilopanga kulitangaza siku ya Ijumaa Agosti 5, 2022.

Alisema, anaye mpenzi na asingependa kuulizwa kuhusu Rayvanny ambaye taarifa zinaeleza kuwa walishaachana na sasa kila mtu ana maisha yake.

“Nina boyfriend, nisingependa kumuongelea Rayvanny.”

Hata hivyo, Paula hakuweka wazi kama huyo mpenzi aliyenaye kama ndiye Rayvanny au ni mwingine tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live