Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula: Niacheni na mambo yangu

Therealpaulahkajala Paula: Niacheni na mambo yangu

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paula Paul Matthyasse; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) na ni mtoto wa staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na producer maarufu P Funk Majani ambaye anasema kuwa, hivi sasa ameangalia ustaraabu mwingine kabisa na siyo mambo ya uhusiano wa kimapenzi.

Paula au Pau anasema kuwa, anachoomba watu wamuache na mambo yake kwani yupo bize kinoma.

Paula anasema kuwa, kila jambo lina wakati wake hivyo na yeye yuko bize na mambo yake mengine kabisa ya maisha yake kwa sababu kuna muda unafika na vitu vinabadilika.

“Kila jambo na wakati wake na maisha yanabadilika siku zote. Kwa sasa nimeweka nguvu kwenye maisha yangu hivyo watu waniache na mambo yangu,” anasema Paula ambaye Ijumaa iliyopita alifungua duka lake la nguo na maisha yanaendelea.

Hata hivyo, Paula hakutaka kuweka wazi kuhusu uhusiano wake na msanii Rayvanny ambaye wanadaiwa wameachana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live