Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula: Naongea na baba fresh tu!

P Funk Na Paula Paula na baba yake

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo maarufu Bongo, Paula Kajala ameweka wazi kuwa ana uhusiano mzuri kati yake na baba yake mzazi P-Funk Majani.

Binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja amefichua kwamba huwa anawasiliana vyema na baba yake na hata kuonana naye mara kwa mara.

"Tuko sawa. Kila siku tuko sawa. Tunaongea. Hata nilikuwa napanga kwenda kwake wiki iliyopita. Anakaa Arusha sasa hivi," Paula alisema jana Jumatano wakati wa mahojiano na Wasafi Media.

Mwanamitindo huyo alidokeza kuwa baba yake huyo atahudhuria hafla ya 'Pink Friday Celebration' ambayo itafanyika Ijumaa.

Pia alifichua kuwa ataitembelea familia ya baba yake hivi karibuni na kubainisha kuwa kuna uhusiano mzuri kati yake na wadogo zake kutoka upande huo.

"Huwa tunaongea. Tunafanya video call. Tunazungumza. Huwa tunakutana mara nyingi. Hata nilikuwa naishi nao," Alisema.

Mwezi uliopita Majani pia alifunguka kuhusu uhusiano wake na bintiye huyo wa miaka 20 na kuweka wazi kwamba huwa wanajuliana hali mara kwa mara na hata kukutana kwa wakati mwingine.

Mtayarishaji huyo akizungumza na waandishi wa habari mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Paula alimtakia binti huyo wa kheri na kumtaka afuate moyo wake katika shughuli zote za maisha.

"Nipo kwa ajili yake siku zote. Siku hizi tunaongea vizuri sana. Tunaenda vizuri na amekua. Ameanza kuwa mzima," Alisema Majani.

Mzazi huyo mwenza wa Kajala Masanja hata hivyo alifichua kuwa hakuna uhusiano mzuri kati yake na muigizaji huyo. Majani alidai kuwa mchumba huyo wa sasa wa Harmonize amekuwa akipuuzilia ushauri wake hasa kuhusu malezi ya binti yao.

"Paula bado mdogo, ana nafasi ya kubadilisha tabia. Mama yake yule hapana. Kwa kweli sisi hatuongei. Sihitaji kuongea naye tena," alisema P Funk.

Pia aliweka wazi kuwa kwa muda mrefu hakujakuwa na hali ya kuelewana kati yake na Kajala.na kufichua kuwa kwa sasa hata hazungumzi naye.

"Mama (Kajala) ni sumu. Lazima izingatiwe niko kwenye ndoa miaka nane na mtu ambaye nimekuwa naye miaka 12, kanizalia watoto watatu. Sasa kama mtu ako na drama unaepuka kidogo," P-Funk alisema.

Kwa sasa Majani yupo kwenye ndoa nyingine huku Kajala akipanga kufunga pingu za maisha na Harmonize hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live