Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula, Fahyma wamponza Rayvanny

Rayvanny Fahyma Paula D Paula, Fahyma na Rayvanny

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rayvanny au Chui; ni msanii mwingine mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye amejikuta akishambuliwa, kisa ex-wake, Paula Kajala na baby mama wake, Fahyma.

Hii ni baada ya kudaiwa kuachia nyimbo ambazo zina vijembe ndani yake tangu alipotangaza kujiondoa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Katika moja ya nyimbo zake ambayo amemshirikisha msanii G Nako, Rayvanny anarusha vijembe kwamba inakuwaje mtu umeshaachana naye, halafu bado anakufutailia ikidaiwa hapo anamlenga Paula ambaye aliachana naye hivi karibuni.

Kufuatia kuandamwa na maneno mengi kwamba, kuna kitu hakipo sawa, ndipo Rayvanny akaamua kuwatolea uvivu baadhi ya wakosoaji wake akiwataka kunyamaza kwani anafanya muziki wake kwa ajili ya watu wake na hana vita na mwanamke yeyote duniani.

“Nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu wangu na sina vita na mwanamke yeyote duniani, tusipangiane.

Baada ya kuachana na Paula, Rayvanny alirudi kwa Fahyma kwa ajili ya kumlea mtoto wao wa kiume aitwaye Jaydanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live