Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula, Fahyma vita upyaaaaa!

Paula Awafokea Paula na Fahyma

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rayvanny au Vanny Boy; ni supastaa mwingine wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye miezi michache iliyopita alithibitisha kuachana na mpenzi wake ‘mchepuko’, mrembo Paula Kajala.Wakati Rayvanny au Chui akiachana na Paula alisema kuwa aliona mapenzi yao hayakuwa na afya njema.

Baada ya kutengana ndipo tetesi zikaibuka mitandaoni kuwa, Rayvanny ameamua kurejea kwa baby mama wake, Faima Msangi almaarufu Fahyvanny au Fahyma.

RASMI RAYVANNY YUPO KWA FAHYMA

Gazeti la IJUMAA linakuthibitishia kwamba ni kweli Rayvanny na Fahyma wapo pamoja na wanalea vizuri mtoto wao wa kiume aitwaye Jaydanny baada ya kutengana kwa takribani miaka miwili; kumbuka wazazi hawaachani, wanatengana tu huku wakiendelea kulea mtoto au watoto wao.

Katika hali ya namna hiyo, taarifa za ndani zinasema kuwa, Paula na Fahyma wapo kwenye vita nzito na mpya kwa sababu ya penzi la Rayvanny. Paula na Fahyma wameendelea kutupiana vijembe na michambo kwa kupitia mitandao ya kijamii katika kile ambacho kimeonekana kuwa ni vita ya wivu wa penzi la Rayvanny.

PAULA HAJAKUBALI

Katika moja ya posti zake, Fahyma anatamba kwenye video akiwa na Rayvanny; lengo lake likiwa ni kumchokoza Paula ambaye anaonekana hajakubali kuvunjika kwa penzi lake na Rayvanny. Paula ambaye si mchache wa maneno ya shombo amejibu vikali mapigo ya Fahyma huku akimuita mjinga ambaye hana akili ili kumkomesha kufanya vitu kama hivyo vya kujiposti na Rayvanny, jambo ambalo anasema ni la kitoto na kipumbavu.

Kama mpaka sasa kwa umri huo bado unaposti picha kwa status ili kumuumiza mtu, unahitaji elimu ya memkwa kwa sababu huna akili,” Paula ametupa bomu hilo kwenye kambi ya jeshi la Fahyma.

Kwa muda mrefu, Paula na Fahyma hawapo kwenye maelewano kwa kile ambacho kambi ya Fahyma

inadai kwamba, Paula ndiye alivuruga penzi la ‘mkuu wao’ na Rayvanny kabla ya kufanikiwa kumrejesha jamaa huyo na kuanza tambo zake kama zamani kuwa, mtoto wa Kitanga huwa haachiki!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live