Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paul Mihambo: Fundi wa reggae tangu mwaka 1996 mpaka leo anakiwasha

Paul Mihambo Paul Mihambo.

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo hii kupitia Msasa Online tunakuletea moja ya wasanii wakongwe walio na uwezo mkubwa haswa kwenye kubeba maana nzima ya sanaa ya Tanzania.

Kutana na "Paul Mihambo" msanii anaeimba muziki aina ya Reggae, ambaye alifanikiwa kuingia kwenye vinyang'anyiro vya tuzo za Tanzania Music Awards 2023 akiwa kwenye kipengele cha Wimbo bora wa Reggae wa mwaka.

Kazi yake ya usanii, alianza kitambo sana akiwa anasoma Bagamoyo secondary miaka ya 1996 akiwa kidato cha kwanza na baada ya kuja kwa mradi uliokua unaitwa TUSEME walikua wanachunguza kwa nini elimu inashuka nchini kwa hiyo na Mihambo, alikua moja kati ya washiriki waliokua wakifikisha ujumbe kwa kupitia muziki wa Reggae na kukaandaliwa Tamasha lililofanyika Chuo kikuu cha Dar Es Salaam, katika ukumbi wa Nkuruma hapo ndio alipoanza kuonesha kipaji na uwezo wake rasmi.

Baada ya kumuuliza juu ya mafanikio yake Paul Mihambo alisema, "Nimefanikiwa kwa kiwango cha kati maana nia na madhumuni ni kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa hilo nimefanikiwa kwa kupitia nyimbo ninazotoa ndio maana nasema ni kiwango cha kati ili niweze sasa kufanikiwa na huu mziki inatakiwa ifike mahali, sasa muziki ninaofanya uweze kunilipa pia hayo ni mafanikio ya pili ambayo ndio niko napambana nayo kwa kujitafuta"

"Changamoto kubwa zaidi ni katika promotions Music wa Reggae ninaofanya haupati Airtime ya kutosha kama miziki mingine kwa hiyo hii ni changamoto kubwa ninayopitia inayonifanya nishindwe kutimiza malengo ya kuupeleka muziki wangu wa Reggae mbele zaidi kwa hiyo hata kuji brand kupitia muziki wa Reggae inaleta ugumu lakini bado naamini kwenye mafanikio kupitia muziki wa Reggae".

Baada ya hayo tulitaka kujua kwanini alichagua muziki huo wa Reggae naye alijibu, "Muziki ni wito na ni taranta yangu kwa hiyo kwangu upo kwenye damu na ndio maana sijauacha mpaka Leo hii na ninaamini katika muziki huu kwangu itakua fursa tena ya biashara maana Muziki ni biashara pia ndio maana nikaamua kuendelea kufanya hii ni taranta yangu pia".

Nje ya kazi ya sanaa, Paul Mihambo ni Mkemia wa Madini na amefanya kazi sehemu mbalimbali kama Buzwagi Gold Mine, Bulyanhulu Gold Mine, Mbeya Cement na sasa Singida Gold Mine kwa fani hiyo hiyo ya Ukemia.

Kuhusu malengo yake esema hivi, "Malengo yangu ni kuutangaza muziki wetu wa Bongo Reggae kimataifa na kuufanya uwe fursa na kuniingizia kipato kwa kueleimisha Jamii".

Asili yetu, Tenda Wema, Amani, Jah of mercy, Usalama Barabarani, Rafiki Mnafiki, Inuka simama, Kubali Matokeo, Ndoto yangu, Darling, Fitina Makazini, Katiba Mpya, Nyota, Salamu zako, ni baadhi ya kazi bora kutoka kwake Paul Mihambo alizowahi kufanya na zikawa na mapokezi chanya kwa kuleta matunda kwenye historia ya sanaa kwenye maisha yake na mashabiki pia.

Kuhusu mapendekezo yake kwenye kazi ya sanaa Paul kasema kwamba, " Viongozi na Wadau mbalimbali wa sanaa, Wausapoti pia Muziki wa Reggae Bongo Reggae kama aina nyingine wanavyosapoti pia mapromoters waweke macho kwenye muziki wa Bongo Reggae ili tuweze kuutangaza kimataifa pamoja na kuaandaa matamasha ya Reggae na wadhamini wajitokeze kwa wingi".

"Mashabiki zangu wanipe support kwa kusikiliza kazi zangu pamoja na ku subscribe katika channel yangu ya YouTube ku like na kuacha comments ili tuweze kuufikisha muziki wa Reggae mbali zaidi", alimaliza kwa kusema hivyo Bwana Mihambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live