Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Patrick Kanumba: Aslay mshikaji wangu tangu tuko watoto

Aslay Patty Patrick Kanumba: Aslay mshikaji wangu tangu tuko watoto

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa Filamu nchini, Othman Njaidi 'Patrick Kanumba' amesema kuwa yeye na staa wa muziki nchini, Aslay Isihak ni washkaji tangu wakiwa wadogo.

Patrick amesema kuwa, yeye na Aslay wamekuwa pamoja huku akiongeza kuwa staa huyo alimshawishi na yeye kuwa staa kupitia tasnia ya filamu jambo ambalo amefanikiwa kutimiza.

"Nimekuja kumsapoti Aslay kwenye show yake ya kusherehekea miaka 10 kwenye muziki kwa sababu mimi na yeye tumetoka mbali, sisi ndio wasanii tulioanza kuwa maarufu na kuonekana kwenye TV tukiwa wadogo mpaka sasa tumekuwa mastaa wakubwa.

"Hii inaonyesha ni kiasi gani tumekuwa wachapakazi na kuwajibika kwenye vipaji vyetu"

"Mimi wakati nakua nilianza kuwa maarufu nikiwa mdogo sana, nilimfahamu Aslay nikiwa na miaka 11 tu nikasema angalau nitakuwa na mwenzangu ambaye ni mtoto na anaonekana kwenye TV, alinitia moyo kuona sikuwa peke yangu.

"Kulikuwa na watoto wengi waliokuwa wanaonekana kwenye TV lakini mimi nilikuwa namuangalia zaidi Aslay na kwa bahati nzuri wote tumekuwa maarufu japo yeye kanizidi umri ila naendelea kujifunza mengi kutoka kwake," amesema Patrick Kanumba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live