Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Patricia Hilary ageukia filamu

Wed, 4 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unamjua msanii aliyewahi kutamba na wimbo ‘Njiwa Peleka Salam’ Patricia Hillary ambao hadi leo ukichezwa  ukumbini watu husimama, basi anakuja kivingine.

Akizungumzia hilo katika mahojiano yake na Mwananchi,  jana Jumanne Septemba 3, 2019, Patricia alisema mashabiki wake wamtarajie kumuona kitofauti hivi karibuni na hii ni baada ya kushirikishwa katika kucheza filamu na msanii Ahmed Salim ‘Gabo’.

Alisema tayari ameshaanza kupiga picha za filamu hiyo ambapo anacheza kama Katibu muhtasi wa mkuu wa wilaya huku akieleza kuwa anajisikia faraja kwa kitendo cha Gabo kumuona anafaa kuigiza.

 “Sina budi kumshukuru  Gabo kwa kuona upande wangu mwingine na tayari nimeshaingia ‘location’ na kupiga picha za scene zisizopungua nne na bado tunaendelea.”

“Kwa sababu nina kipaji cha kuzaliwa, nimemudu nilichoelekezwa japokuwa haikuwa kazi rahisi kwangu kwani nilishaozea kuimba na si kuigiza,” anasema.

Kwa upande wake, Gabo alisema ameamua kumchukua mama huyo kama njia moja ya kuonyesha jamii ukubwa aliokuwa nao katika sanaa ya Tanzania.

Pia Soma

Advertisement   ?
Gabo alifafanua kwamba kuna wasanii wakubwa wa nchi hii watu wameshindwa kuwatumia vilivyo, kupitia Patricia anajua ataacha somo kwa wale ambao wamekuwa wakiwachukulia poa  wasanii wa aina yake.

“Nasikitika sana kuna watu wa ajabu tumekuwa tukiwapa jina la wasanii wakati kuna wasanii wenyewe halisi ambao wakisimama unakubali kweli huyu msanii, ni wakati wa kuwapa heshima yao hata kama umri umeshawapiga mkono kwani msanii  kipaji chake hufa pale anapoondoka duniani, ”amesema.

Mbali na kibao cha njiwa nyimbo nyingine alizowahi kutamba nazo ni pamoja na ‘Chura’ na  “Ni Mdodo’ inayopigwa mara nyingi kwenye harusi zinazolihusisha kabila la wasambaa.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz