Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Patoranking afichua sababu za ukimya wake kwenye muziki

Patoranking 696x384 Patoranking afichua sababu za ukimya wake kwenye muziki

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka Nigeria Patrick Nnaemeka 'Patoranking' amefichua kuwa ukimya wake kwenye muziki ulitokana na yeye kuwa masomoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Patoranking ame-share picha zikifichua kuwa siku chache zilizopita alitunukiwa Shahada 'Degree' kutoka katika Chuo Kikuu cha #Harvard nchini Marekani akiwa ni mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la BEMS 2024.

Patoranking alieleza kuwa yeye na wengine 35 wamepata Degree in Business, Entertainment, Media, and Sports (#BEMS)’.

Mara ya mwisho #Patoranking kuachia ngoma ni miezi saba aliyopita, aliachia video ya wimbo wake wa ‘Babylon’aliomshirikisha #Victony ukiwa na zaidi ya watazamaji milioni 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live