Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Padri ashambuliwa kisa mapenzi ya jinsia moja

Padre Ke Padri ashambuliwa kisa mapenzi ya jinsia moja

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Padre wa Kanisa Katoliki, Ambrose Kimutai kutoka katika Dayosisi ya Kericho kaunti ya Bomet, amekosolewa vikali kutokana na kile wengi walikitaja kama msimamo tofauti wa kanisa.

Kimutai alisema anaunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Upeo na kuwahimiza Wakenya kupenda na kuheshimu jamii ya LGBTQ akidai ni funzo katika biblia.

Kulingana na padri huyo, amesema jambo moja ambalo jamii hiyo ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ilitaka ni uhuru wa kutangamana na kukusanyika pamoja.

Kimutai alisema LGBTQ wanapaswa kupewa haki na uhuru wa kutangamana mradi tu hawavunji sheria.

"Hawakwenda mahakamani kwa sababu walitaka kuruhusiwa kuoa au kuolewa, walienda mahakamani kwa sababu walitaka kuruhusiwa kuwa na muungano wao na bodi ya NGO ilikataa kuwasajili," alisema.

Aliongeza kuwa hawezi kuwazuia kwani haelewi kabisa walichokuwa wakifanya na mahakama iliamua hivyo watu lazima waheshimu uamuzi huo.

Kasisi huyo mwenye utata aliwaomba viongozi wengine wa kidini kuzingatia kufundisha maadili katika familia na umuhimu wa familia.

Mahakama ya Upeo Katika uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Upeo mnamo Ijumaa, Februari 24, iliamua kuwa jamii ya Wasagaji, Mashoga na Wanaobadilisha Jinsia (LGBTQ) ina haki ya kusajili shirika lao lisilo la kiserikali (NGO) nchini Kenya.

Japo mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini Kenya, mahakama ilisema kuwa hakuna sheria inayozuia jamii ya LGBTQ kujumuika pamoja.

Hata hivyo, siku ya Jumapili, Februari 26, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi alisema kuwa uamuzi huo ni kinyume na maadili ya jamii. Muturi alisema Wakenya wanapaswa kuruhusiwa kutoa maoni yao kupitia ushirikaji wa umma kwani suala la LGBTQ lina uzito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live