Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacha wa Michael Jackson apatikana

Pacha Wa Michael Jackson Apatikana Pacha wa Michael Jackson apatikana

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na kuwepo kwa mpango wa kutengenezwa filamu ya mfalme wa Pop Michael Jackson (MJ) huku akisakwa mtu ambaye atafanana na kuwa na miondoko kama msanii huyo, hatimaye mtu huyo amepatikana ambaye ni Mpwa wa MJ aitwaye, Jaafar Jackson.

Kwa mujibu wa muongozaji Antoine Fuqua na mtayarishaji Graham King wa filamu hiyo, wameeleza kuwa japo Jaafar anauwezo mdogo katika uigizaji lakini ndiye mtu pekee ambaye amebeba uhusika wa #MJ ipasavyo, hivyo wanafuraha sana kumfufua mwanamuziki huyo katika tasnia ya uingizaji.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Jaafar ame-share picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye mapozi ya #MJ akiambatanisha na ujumbe ukieleza kuwa ni furaha na heshima kubwa kwake kutekeleza uhusika wa mjomba wake Michael.

Filamu hiyo ya ‘#Michael’ ilipangwa kuazwa kurekodiwa mwaka 2023 lakini kufuatiwa na changamoto, imeanza kurekodiwa mwishoni mwa Januari 2024 huku ikitarajiwa kuachiwa rasmi Aprili 18, 2025.

#JaafarJackson (25) ni mwanamuziki na dansa ambaye alianza kuimba rasmi akiwa na umri wa miaka 12, na kujulikana rasmi mwaka 2019 baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Got Me Singing’, huku wimbo wake wa mwisho ameachia jana Februari 14 uitwao, ‘Rebirth of Michael’.

Ikumbukwe kuwa Michael Jackson alizaliwa mwaka 1958 na kufariki dunia mwaka 2009. Alitamba na nyimbo zake kama vile Smooth Criminal, Thriller, Will You Be There

Chanzo: www.tanzaniaweb.live