Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

POLISI: Waliomuua Rapa AKA walikusudia

AKA Dead POLISI: Waliomuua Rapa AKA walikusudia

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Afrika Kusini wamesema kuwa ushahidi uliokusanywa hadi sasa unawaongoza kuamini kuwa kifo cha rapa maarufu AKA kilikuwa ni cha mauaji yaliyokusudiwa.

Mkuu wa Polisi wa KwaZulu Natal Nhlanhla Mkhwanazi amesema kuwa ”mtu mwenye silaha alimsogelea AKA akitokea nyuma na kumpiga risasi kwa karibu sana upande wa kichwa chake”.

”Tunajua dhumuni kuu lilikuwa kumuua AKA, risasi za muuaji wa pili zilizokuwa zikitawanya watu zilimuua rafiki wa AKA mpishi mashuhuri Tibz Motsoane lakini hazikuwa zimemlenga mtu, hivyo zingeweza kumpata mtu yoyote aliyekuwa karibu”

Wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi kupata picha kamili ya kilichotokea kwa AKA ambaye jina lake kamili ni Kiernan Forbes, baba yake mzazi amewaomba watu kuacha kubahatisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Vilevile amewashukuru kwa salamu zao na sapoti kubwa ambayo hadi sasa inawafariji sana.

Polisi wamesema wazi kuwa wamekwisha watambua watu wawili waliopiga risasi na wanaendelea kujaribu kuwatambua watu wengine wote waliokuwa kwenye eneo husika wakati wa tukio, hata hivyo mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa.

Ijumaa ya tarehe 17 Februari kutakuwa na tukio la kumbukumbu kwa ajili ya umma huko Johannesburg, AKA atazikwa Jumamosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live