Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P-Unit: Tulimnyima kolabo Diamond

Diamond Boneye 821 P-Unit: Tulimnyima kolabo Diamond

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya Memba wa kundi la #PUNIT, Kundi la muziki la Kenya amefunguka kuwa kipindi kundi hilo linafanya vizuri walimkatalia Staa wa Muziki Diamond Platnumz awashirikishe katika wimbo wake.

Boneye alisema; "Tulinyima kolabu Diamond, kuna time Diamond alitungojea kwa lobby Dar es Salam kwa saa nne tukiwa kwa hoteli, alikuwa anataka tufanye kolabo na yeye na kutamnyima,”

Mbali na hivyo amefunguka kuwa kinakipindi walisafiri na kuja Dar es salaam na Staa #Diamond aliwasubiri njee ya Hotel walioyokuwa wamefikia kwa masaa manne akisubiri kuwaomba awashirikishe kwenye ngoma yake na walikataa kwani sio kila msanii anatakiwa kupewa kolabo.

Boneye anasema kuwa Diamond Platnumz alitaka awashirikishe katika wimbo wake wa #NtampataWapi ngoma ambayo iliachiwa rasmi Novemba 20, 2014 na kufanya vizuri na mpaka sasa inawatazamaji zaidi ya Milioni 45 katika mtandao wa Youtube.

"But actually, nakumbuka alikuwa ameandika hiyo ngoma already na akatuambia ningependa kufanya collabo na nyinyi and akaniimbia mpaka chorus ya hi ngoma. Na hiyo ndoma ni Nitampata wapi kama Yule?

"Actually alisema anataka ikuwe P-Unit featuring Diamond but hapo hapo bado ndo nilimshika mko nikamuingiza kwa van ya MTV na hiyo ndo opportunity alipata tukaenda na yeye Lagos akatuimbia Chorus ya Kare,”

Mbali na hivyo #Boneye anasema licha ya kuikosa kolabo na P-UNIT lakini walimsaidia kufikia uongozi wa Rapa #RickRoss na kufanya nae kazi.

"Na hapo bado ndo aliipata opportunity ya kumeet Management ya Rick Ross na hivo ndo alipata collabo na Rick Ross. So si ati opportunity ilipotea juu hakufanya collabo na P- Unit. So alipata opportunity,”.

Una Maoni gani kwenye hili?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live