Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P – Funk na Kajala wapewe maua yao

Paula Marioo Pfunk Kajala P – Funk na Kajala wapewe maua yao

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana Aprili 18 ilikuwa siku kubwa kwa Mario na Paula. Lakini pia ilikuwa furaha kwa familia zote mbili na kwa upande wa wazazi wa Paula, P -Funk na Kajala ilikuwa furaha mara mbili.

Kumuona mtoto wao katika jambo lake la muhimu na zaidi kutarajia mtoto wake wa kwanza.

Katika comments mbalimbali mitandaoni watu wengi wamefurahishwa na uwepo wa baba yake Paula katika shughuli hiyo ‘baby shower’ ya Paula. P – Funk alitoa maneno ya busara kwa wawili wao na kuwapa ‘tips’ kidogo ya namna ya kumlea mtoto wao atakapozaliwa kama kumuweka mbali na utandawazi. Majani pia aliwaombea wawili hao mahusiano ya kudumu kama ndoa yake ilivyodumu.

Kubwa zaidi pia lililovutia hisia za watu wengi ni namna mama yake Paula Kajala Masanja alivyosema wazi kwamba anamuomba radhi mzazi mwenzake. Akieleza zaidi anasema kuna wakati walipingana kwenye baadhi ya mambo na Majani kama baba kuna vitu alikuwa havipendi na yeye (Kajala) alikuwa anakosea na alimuomba msamaha.

Lakini jambo lingine ni mahusiano mazuri kati ya Kajala na mke wa P -Funk, Samira. Kajala pia alimshukuru na kusema wakati wote walipokosea Samira alikuwa kimbilio kuweka mambo sawa.

Mke huyo wa Majani alishukuru kwa kuwa sehemu ya shughuli hiyo na kumwambia Paula anampenda sana na siku zote atakuwa karibu nae. Huku akimtania Mario endapo atazingua basi ‘atakula makwenzi’.

Waswahili wanasema kuachana sio ugomvi tena hasa mkiwa na mtoto. P -Funk na Kajala wameonyesha mfano wa kuigwa kwamba malezi baada ya kuachana yanawezekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live