Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P Funk alivyokimbia studio kisa Madilu System

Madilu  Dsc P Funk alivyokimbia studio kisa Madilu System

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uliwahi kusikia ule msemo hata uchawi unazidiana? Hilo ndio lililomtokea P Funk, hakuna anayebisha juu ya uhodari wake wa kuzalisha muziki.

Lakini kuna tukio lilitokea ni Mwanamuziki wa kimataifa ambaye ni hayati kwa sasa James 'Cool James' Dandu alienda Bongo Records na mwanamuziki mkubwa sana Afrika na dunia si mwingine ni hayati Madilu 'Ninja' System , kwa ajili ya kurekodi wimbo 'Mamou Rmx'.

P Funk alipomwona Madilu na aina ya muziki anaoufanya akajua hapa kazi ipo, ila akaona sio shida yupo hapa Alain 'Cente' Mapigo mkali wa hizo kazi atamaliza shughuli.

P akamkabidhi kazi hiyo Alain Mapigo na Alain bila tashwishwi akafanya 'unyama' wake na kuipika ngoma ya kimataifa 'Mamou Rmx' ya Cool James Ft Madilu System.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live