Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P Funk: Wasanii wanapenda kulalamika lakini vitendo hakuna

Majani 2 P Funk P Funk Majani

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Prodyuza mkongwe wa muziki Bongo, P Funk Majani amesema wasanii wengi wa muziki wa Bongo Fleva wanapenda kulalamika kuhusu haki zao lakini wakipewa fursa ya kutoa maoni yao ili sharia ama kanuni zitungwe kuboresha wanakwepa.

P Funk amesema hayo wakati akihojiwa na wanahabari wakati kamati Maalum iliyoudwa na COSOTA kukusanya maoni na kushughulikia masuala ya hakimiliki za wasanii ilipokutana kujadili, ambapo P funk ni miongoni mwa wanakamati na viongozi wa kamati hiyo.

"Tunafahamu mikutano mikubwa ikitokea, wasanii wakubwa huwa hawapendi kujitokeza, ninachoomba kwao, tukipokea maoni, uamuzi ukatoka sio kwamba mje mlalmike kwamba hamjashirikishwa. Ni muhimu kutambua hilo, wana nafasi ya kuingia mtandaoni na kuweka maoni yao ama kupitia namba ya WhatsApp ambayo imewekwa ili baadaye tuepuke lawama.

"Kwenye sekta ya Bongo Fleva ndio utamaduni wetu, wanapenda kulalamika lakini vitendo hatuna, ndivyo tulivyo… tumeshafeli huko nyuma, lakini kwa sasa hivi tumejifunza vya kutosha hatuko tayari kufeli tena, tunarekebisha na tutafanikiwa.

"Wasanii mnapokuwa na umoja mnakuwa na sauti moja na fikra moja, ni vizuri tujifunze kukaa chini ya vyama, kwa sababu hata mkiitwa leo na Mhe. Rais Samia Suluhu mkazungumze naye kutoa changamoto zetu au kujadili mambo muhimu kuhusu sanaa, hamuwezi kwenda wote, watakwenda viongozi wenu ambao ndio sauti yenu kwenda kuwawakilisha.

"Tumekusanya mirabaha kwa muda mrefu, saa nyingine ilikuwa ikikusanywa lakini mgao hautoki mara utoke, lakini sasa hivi vitu vinakwenda kwa kasi sana. Vitu vikisemwa vitafanyika, vinafanyika. Kwa miaka ya nyuma watu kuelewa maana ya mirabaha na hakimiliki zao ilikuwa ngumu sana, hata wasanii sasa hivi wanaanza kueleawa," amesema P Funk.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live