Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P Funk: Sihitaji kuongea na Kajala tena

P FUNK, KAJALA PAULA P Funk: Sihitaji kuongea na Kajala tena

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Procuder legendary wa muziki wa Bongo, P Funk ‘Majani’ amesema kwa sasa hahitaji kuzungumza na mzazi mwenzake, Kajala Masanja kwani amekuwa akimshauri mambo mengi kuhusu mtoto wao, Paula lakini anayapuuzia na mwishio wa siku yanakuja kuwa na madhara kwa mtoto.

Majani amesema hayo hivi karibuni wakati akifanyiwa mahojaiano na vyombo vya habari huku akisema kuwa kwa sasa Pula amekua na wanaongea vizuri, hivyo hana haja ya kuongea na Kajala badala yake atazungumza na Paula moja kwa moja kama kuna jambo la kumshauri.

P Funk amedai kuwa Kajala amekuwa ni mtu wa drama na ameshindwa kubadilisha tabia, lakini kwa vile mwanaye sasa anajitambua, yeye ataendelea kumpa ushauri mwanaye. “Mama ‘is toxic’ mimi na yeye hatuelewani, mimi niko kwenye ndoa na mwanamke kwa miaka 12 na amenizalia watoto watatu, kama mtu ana drama una-avoid kidogo. Sababu unapotoa ushauri, unamwambia hiki kitakuja kukugeukia, yeye hajali.

“Paula bado ni mdogo, ana nafasi ya kubadilika tabia, lakini mama yake yule ‘let it be’ kwa kweli sisi hatuongei, sihitaji kuongea naye tena, sababu Paula ana umri tayari ambao ni mtu mzima. Kama kuna salam tutasalimiana, kama tutaonana sehemu tutasalimiana,” amesema P Funk.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live