Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P Diddy kupokonywa funguo za New York

Attachment Diddy Key To The City P Diddy kupokonywa funguo za New York

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo yanazidi kuwa magumu kwa upande wa Rapa Diddy mara baada ya taarifa iliyotoka hivi karibuni ya kwamba uwenda akavuliwa heshima ya funguo ya mji wa New York (Key to the city)

Hii imekuja mara baada ya meya wa mji huo mr Eric Adams kuelezea ya kuwa wamesikitishwa na tukio linaloonekana kwenye video ikimuonyesha Diddy akimfanyia unyanyasaji aliyekuwa mpenzi wake Cassie, tukio lilofanyika machi 2016 na uwenda ikasababisha Diddy kupoteza heshima ya funguo wa mji wa New York.

Wakati alipokuwa anafanyiwa mahojiano na kituo cha runinga cha @pix11news, Meya alisema kuwa utawala wake unachambua kwa uangalifu tukio hilo na kufanyia uchunguzi na huwenda wakafanya maamuzi ya hata kurudisha ufunguo wa Diddy kwa jiji.

Heshima hiyo ya funguo wa mji (key to the city) Rapa Diddy alikabidhiwa na meya huyo siku ya septemba 15, 2023 katika mtaa wa times square mjini New York nchini marekani kama heshima ya ushawishi wake katika jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live