Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P Diddy atajwa kuhusika kifo cha Tupac

Diddy X Tupac P Diddy atajwa kuhusika kifo cha Tupac

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Duane “Keffe D” Davis, Mtuhumiwa wa Mauaji ya Rapper Tupac Shakur ameshitua ulimwengu baada ya kukiri kwamba ni kweli alimuua Tupac lakini ameweka wazi kuwa alilipwa Dollar Milioni moja kwa ajili ya kutekeleza mauaji hayo.

Mtuhumiwa wa Mauaji hayo mara nyingi akiwa Mahakamani Las Vegas amekiri kwamba P Diddy alimuomba amuue Tupac Pamoja na Suge Knight (Aliyekuwa Mkuu wa Label aliyokuwepo Tupac "Death Row")

Tupac alishambuliwa kwa risasi Tarehe 7 Septemba 1996 baada ya gari alilokuwa amepanda kusimamishwa kwenye taa nyekundu Las Vegas. Kwenye gari hilo alikuwa akiendeshwa na Suge Knight. Tupac alifariki baada ya Siku Sita (Tarehe 13 Septemba 1996)

Kwa miongo kadhaa P Diddy ni miongoni mwa watu wanaohusishwa na Kifo cha Tupac ila mpaka sasa hakuna mahakama iliyothibitisha dai hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live