Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P Diddy ajiuzulu uenyekiti wa Revolt TV

P Diddy Ajiuzulu Uenyekiti Wa Revolt TV P Diddy ajiuzulu uenyekiti wa Revolt TV

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Kufuatia kesi tatu za unyanyasaji wa kingono dhidi yake, msanii maarufu wa rap Sean "Diddy" Combs amejiondoa kama mwenyekiti wa mtandao wa TV alioanzisha pamoja na mfanyabiashara mwenzake

Revolt ilisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba nyota huyo wa hip-hop hakuwa na "jukumu la kila siku katika biashara".

Msanii wa R&B Cassie alimshutumu Bw Combs kwa ubakaji na unyanyasaji, lakini wawili hao walisuluhisha kesi hiyo mara baada ya kuwasilishwa.

Siku chache badaye wanawake wengine wawili wakajitokeza.

Bw Combs amekanusha madai hayo, akisema matukio ya hivi punde ni njama ya "kumlaghai".

Revolt iliweka katika mitandao ya kijamii Jumanne kuhusu hatua ya Bw Combs kujiuzulu, akiandika: "Ingawa Bwana Combs hapo awali hakuwa na jukumu la kufanya kazi au la kila siku katika biashara, uamuzi huu unasaidia kuhakikisha kuwa Revolt inabaki kulenga dhamira yetu."

Kabla ya Bw Combs kujiuzulu kwa muda, Dawn Montgomery, mtangazaji mwenza wa podcast ya Revolt Monuments to Me, alitangaza kuwa hatajisajili kwa msimu wa tatu wa kipindi hicho.

Bi Montgomery aliandika kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter: "I am a SA survivor & I haiwezi kuwa sehemu ya show ambayo inapaswa kuinua wanawake weusi wakati @Diddy anaongoza kampuni."

Bw Combs alianzisha mtandao wa televisheni na tovuti ya muziki mwaka wa 2013, lakini bado haijabanika iwapo atarejea kama mwenyekiti.

Hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Sean 'Diddy' Combs kuhusu uamuzi wa kujiuzulu uenyekiti.

Chanzo: Bbc