Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Otile Brown ameshindwa kujizuia kuhusu Abby Chams

Abby Chams Mk Abby Chams

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki nchini Kenya, Otile Brown ameshindwa kujizuia na kufunguka hadharani jinsi anavyomukubali msanii wa kike kutoka Tanzania, mwanadada Abby Chams.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Otile ameonesha kuukubali uwezo wa mrembo huyo kwa ku-share picha ya wimbo wa Rayvanny aliomshirikisha Abby Chams, STAY na kuandika ujumbe unaosomeka;

“Abby Chams Mashallah, Coming to Tanzania anytime Inshallah hopn to meet you queen....” Ujumbe huo umewaaminisha mashabiki kuwa huenda wawili wana mpango wa kuja na wimbo wa pamoja hivi karibuni.

Iwapo Otile Brown atafanikisha suala la kuachia wimbo wa pamoja na Abby Chams itakuwa ni kazi yake ya tatu kufanya na msanii wa Bongo fleva ikizingatiwa tayari ana Kolabo na Ali Kiba na Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live