Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ostaz Juma amlipua tena Zuchu “Siogopi kushtakiwa”

Ostaz Juma Na Zuchu Ostaz Juma amlipua tena Zuchu “Siogopi kushtakiwa”

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mdau nguli wa masuala ya muziki nchini, Ostaz Juma Namusoma ameibuka tena na kumjibu msanii wa WCB, mwanadada Zuchu akidai kuwa wasanii ndiyo chanzo cha kuharibu taswira za wazazi wao kabla ya mashabiki na kuongeza kuwa yeye haogopi kushtakiwa kwani anachokisema ndicho wanachokifanya wasanii hao.

Ostaz Juma amesema hayo kufuatia kauli yake ya awali aliyoufananisha mwili wa Zuchu na mama yake Khadija Kopa huku akimtaka Diamond Platnumz amuoe binti huyo na asimchezee kimapenzi jambo ambalo lilimuibua Zuchu na kudai kuwa hawezi kufumbia macho kwa udharirishaji anaofanyiwa na Ostaz Juma huku akiahidi kumfikisha katika vyombo vya sheria.

“Siogopi, bali naheshimu. Napenda kusema kwamba nashukuru ujumbe wangu unawafikia vizuri na ujumbe wangu na maneno yangu ni darasa kubwa sana kwenu wasanii. Ikiwa ujumbe wangu unawafikia basi ufanyieni kazi.

“Huko nyuma niliwahi kusema kwamba nyie wasanii wa sasa mnaandika nyimbo mbaya na mbovu, mnawadharirisha wazazi wenu. Ikiwa ni moja na wewe mwenyewe uliwahi kuimba kwamba ‘Khadija Kopa zungusha…’ azungushe kitu gani? Ulichokuwa unakitaka mama yako akizungushe kwenye mwili wake ni kitu gani?

“Mnaimba nyimbo na nyie ndio wa kwanza kwa kuwataja wazazi wenu vibaya na kuwadharirisha, na kuzizungumzia familia zenu vibaya, mkitaka kuwaimba wazazi wenu watajeni katika maudhui mazuri.

“Kuna mwingine pia aliwahi kuimba kwamba, ‘Mama Dangote hodari, hodari wa mapenzi…’ ikiwa wewe ni mtoto utajuaje uhodariu wa mapenzi wa mzazi wenu? Mama yenu utajuaje uhodari wake wa mapenzi? Kwa nini?

“Ndiyo maana nasema nyie wasanii ni kioo cha jamii, ikiwa mnahitaji wazazi wenu waheshimiwe, basi mtaonyesha nyie heshima kwanza kwa wazazi wenu mnavyowachukulia, mkiwachukuliwa kawaida hata mashabiki zenu pia watawachukulia kawaida.

“Na kwa nini umechukia sana kuambiwa unafanana na na umemrithi mama yako? Kwa hiyo unalichukia umbo la mama yako? Hupendi kufanana na mama yako? Ulitakiwa usema al hamdu lillahi kama nafanana na mama yangu nitakuwa ni kopi ya mama yangu,” amesema Ostaz Juma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live