Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ostaz Juma Namusoma: Diamond anajidharirisha kwa Zuchu

Ostaz Juma Mondi (1) Ostaz Juma Namusoma vs Diamond

Tue, 6 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mdau nguli wa masuala ya muziki nchini ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa wasanii mbalimbali nchini, Ostaz Juma Nmusoma ameendelea kumkosoa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz akidai kuwa kutoka kimapenzi na msanii wake Zuchu ni kujishuhsia heshima.

Ostaz ambaye amekuwa akimponda Diamond katika kila analofanya, ameibuka na kauli hiyo baada ya picha za Diaomnd kusambaa akicheza na Zuchu kwenye usiku wa uzinduzi wa albamu ya Barnaba.

“Mtu mzima huwezi kujidharirisha na msanii wako stejini mnapigana mabusu mnakumbatiana, ma’ke ni mtoto anaweza akamzaa yule.

“Sasa mtu umeshamsaidia kimuzki amefika hapo alipofika, kama unataka heshima ulitakiwa uijenge heshima yule mtoto, umheshimu kama mzazi wake nay eye akuheshimu kama mlezi wake. Kwa hiyo unachukua asilimia 60 na utamu unakula,” amesema Ostaz Juma.

Hata hivyo, Diamond na Zuchu hawajawahi kutihibitisha kuwa wana uhusiano wa kimapenzi licha ya kuwa karibu muda mwingi kiasi cha kusafiri kwenda mpaka Ulaya kwa ajili ya kazi zao za muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live