Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Oscar Pistorius aachiwa huru baada ya kukaa gerezani miaka 11

Oscar Pistorius Kuachiwa Huru Kwa Msamaha Leo Afrika Kusini Oscar Pistorius

Sat, 6 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mwanariadha wa Olimpiki mwenye ulemavu, Oscar Pistorius ameachiwa hurujana kwa msamaha nchini Afrika Kusini baada ya kukaa gerezani kwa takribani miaka 11 kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Alimpiga mpenzi wake risasi kadhaa kupitia mlango wa bafuni mwaka wa 2013 na kudai kuwa alidhani ni mwizi.

Pistorius, ambaye sasa ana umri wa miaka 37, alipatikana na hatia ya mauaji mwaka 2015 baada ya mahakama ya rufaa kubatilisha hukumu ya awali ya mauaji bila kukusudia.

Hata akiachiwa huru, bado ataishi chini ya masharti magumu mpaka kifungo chake kitakapomalizika mwaka 2029.

Kwa sheria za Afrika Kusini, wahalifu wote wana haki ya kuachiwa huru kwa msamaha mara tu watakapokuwa wametumikia nusu ya kifungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live