Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ommy Dimpozi amuaga Magufuli kwa wimbo

661fa70f081bfba0d1bcf239bca13af8.jpeg Ommy Dimpozi amuaga Magufuli kwa wimbo

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa Bongo Flava, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema kwa alama alizoiacha Rais Dk John Magufuli, ameamua kumuaga kwa wimbo wa Baba Akupokee.

Dimpoz amesema ameamua kuutoa wimbo huo kama zawadi kwa Magufuli ambaye alikuwa sawa na baba kwa jinsi alivyokuwa akijitoa kuhakikisha wasanii wanapata heshima inayostahili.

“Hakika ni pigo kubwa kwa tasnia ya Bongo Flava, alikuwa baba yetu, alikuwa tayari kutusikiliza pindi tulipokuwa tunahitaji msaada kutoka kwake,” alisema.

Alisema ni ngumu kupata tena mtu wa mfano wake ambaye alikuwa tayari kumuona kila Mtanzania akifurahia kuwa raia wa taifa hili.

Ommy Dimpoz alisema anamuombea heri Rais Magufuli huko aendako apate pumziko la milele.

Chanzo: www.habarileo.co.tz