Nyota wa Bongo Fleva, mwimbaji Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anaomboleza kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, Maya Mia (Make Up Artist Mashuhuri) raia wa Macedonia aliyefariki dunia mwishoni mwa wikiendi iliyoisha, ametoa taarifa kuwa ameibiwa kiasi cha Shilingi Milioni 30.
Dimpoz amebainisha hilo kupitia insta story yake ambapo ameeleza, siku ya jana ameibiwa kiasi hicho cha fedha ($13K), ambazo ni sawa na takribani Tsh. Milioni 30+ huku akiongeza kuwa ameamua kumshtakia Mungu kwa aliyetekeleza wizi huo.
"Yani hata sijapoa na msiba, jana nimeibiwa Dola elfu 13, almost Milioni 30 hiyo lakini nimeamua kumshtakia Allah????," amesema Ommy Dimpoz.