Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ommy Dimpoz afunguka kila kitu kuhusu kunyweshwa sumu

Dimpoz Ommy Ommy Dimpoz.

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hit Maker wa #MyQueen, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz kupitia Exclusive interview na #TheSwitch ameeleza kuhusu sakata la kunyweshwa sumu ambalo limekuwa likihusishwa na baadhi ya watu maarufu.

Ikumbukwe kuwa, miaka kadhaa iliyopita, Dimpoz alilazwa ICU nchini Afrika Kusini baada ya kupata kansa ya koo kwa kile kilichoelezwa na madaktari kuwa alikula au kunywa kitu chenye sumu.

“Kuhusu kuwekewa sumu ni watu wanajiandikia tu wala havina ukweli wowote. Madaktari waliniambia umekula au umekunywa kitu ambacho kina simu, mimi nikasema nitajikita kwenye matibabu ili niweze kupona.

“Ukianza kuhangaika na nani amekunywesha sumu utaumiza kichwa sababu huwezi jua sumu ulikula kwa bahati mbaya au ulikula kitu kime expire. Ukizungumzia wivu hata ndugu wanaweza kukuonea wivu au rafiki wa kike. Kwenye circle yetu huwezi kujua nani amekuwekea sumu.

“Kwa vile jambo hilo lilitokea katika kipindi ambacho tulikuwa kwenye ugomvi lazima watu watasema tu kwamba atakuwa ni flani lakini kusema kweli hayo mambo niliachana nayo nikajikita kwenye matibabu na kumwachia Mungu,” amesema Dimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live