Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ommy Dimpoz abariki Basata kufungia nyimbo za wasanii Tanzania

49293 Wasaniipic

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tofauti na wanamuziki wengi wanaopingana na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata)  na mamlaka nyingine kufungia kazi za wasanii zinazoelezwa kukiuka maadili, mwanamuziki Ommy Dimpoz ameunga mkono akisema si sahihi kufanya kazi zinazokiuka mila na desturi.

Baraza la Sanaa nchini limekuwa likiwashughulikia wasanii hasa wanapofanya mambo yanayodaiwa kukiuka maadili ikiwamo mavazi yanayoacha sehemu kubwa za maungo ya wanawake na mashairi yenye lugha chafu.

Akizunguma na Mwananchi jana Machi 28, 2019, Dimpoz amesema kuna wasanii wengi wakubwa Afrika ambao walipenya kimataifa bila kutengeneza nyimbo au video zinazokiuka mila na desturi.

“Mimi siamini katika mavazi kwamba ndiyo silaha inayoweza kumpeleka msanii kimataifa, mwisho wa siku sisi bado ni Waafrika na Watanzania wenye mila zetu na desturi hivyo tunapaswa kuzilinda,” anasema.

Hata hivyo, amesema kuna changamoto ya kudhibiti kazi za aina hiyo katika ulimwengu wa kidijitali hasa pale mamlaka zinapoamuru aina fulani ya nyimbo zipigwe baada ya muda fulani.

Amesema haoni tatizo kwa mamlaka kuwasimamia wasanii kwa kuwa wanatimiza wajibu wao pia amewataka wasanii kutovimbisha msuli.

Related Content

Kuhusu kufanya kazi na Diamond amesema ikihitajika anaweza kufanya naye kazi kwa sababu hana tatizo naye na anaamini naye hana tatizo na hilo.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz