Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ombi la Ray C kwa Rais JPM

984 Sequence 01.Still016 TZW

Wed, 3 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo January 2, 2018 msanii mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva Rehema Chalamila (Ray C) amemuomba Rais JPM kupitisha sheria kama ya Rais Sultan Qaboos wa Oman kwamba hakuna uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke mpaka wafunge ndoa na ikibainika wamekamatwa wapelekwe Segerea.

Rayc C ameandika ombi hilo kupitia ukurasa wake wa instagram  “Mzee mi na shida Moja! hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji Sana!  Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili! Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman!  Hakuna mahusiano ya Kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa! 

“Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila Cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea! Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe! Utakuwa umewanyoosha kisawasawa hawa Wanaume zetu. Tutaheshimiana! #NilivyoamkaLeo Atakaeongea upupu nampa block

Chanzo: millardayo.com