Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Olamide: Nilianzisha lebo ili nitumie pesa zangu

Olamide Net Worth Biography Olamide Gbenga Adedeji.

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa na mwimbaji wa Nigeria, Olamide Gbenga Adedeji anayejulikana kwa jina la 'Olamide', amefichua kuwa alianzisha lebo ya kurekodi ili aweze kutumia pesa zake kwa kuwa zilikuwa nyingi.

Bosi huyo wa lebo ya "YBNL Nation" ambayo inawasimamia wanamuziki wa afrobeat nchini huo 'Fireboy DML' na 'Asake', amekiri uamuzi wake huo umekuwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

"Nilianza tu kukusanya pesa na pesa zilikuwa nyingi sana kwangu. Mimi ni kama sina chochote cha kufanya na pesa hizi zote, ninahitaji kuendelea kusaini watu wapya. Acha nitumie pesa kwa watu, Unajua ni kama njia yangu ndogo ya kurudisha kwa jamii" amepigia mstari 'Olamide'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live