Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ohooo! Kajala amponza Harmonize

Harmonize Na Kajalaaaa Ohooo! Kajala amponza Harmonize

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muandaaji wa Tamasha lililomhusisha msanii Harmonize nchini Qatar, amelalamika kuwa msanii huyo alikiuka makubaliano kadhaa katika kazi yao, ikiwemo kwenda na Kajala Masanja katika tamasha hilo.

Muandaaji huyo anayefahamika kwa jina la Max (Maxwide), amesema kuwa makubaliano yaliyokuwepo baina yake na Harmonize katika Tamasha la AFRO BONGO NIGHT lililofanyika Julai 14, mwaka huu, yalikuwa ni msanii huyo kwenda bila Kajala ili kutoa nafasi kwa mashabiki ambao wangehitaji kupata muda wa kutosha na Harmonize.

Max amelalamika kitendo cha msanii huyo kulazimisha ipatikane tiketi ya ndege kwa ajili ya Kajala ambayo haikuwa katika makubaliano yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live