Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa utamaduni Dodoma afariki dunia ajalini

Ofisa utamaduni Dodoma afariki dunia ajalini

Tue, 7 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Ofisa utamaduni Jiji la Dodoma nchini Tanzania, Willium  Chishosha amefariki dunia katika ajali ya gari wakati akitokea nyumbani kwao Wilaya ya Mpwapwa kwenda Dodoma mjini.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 6, 2020, Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe amesema taarifa za awali walizozipata, Chishosha alipata ajili akitokea nyumbani kwao Wilaya ya Mpwapwa .

“Taarifa za awali zinasema kuwa ofisa huyo alikuwa na mkewe leo, wakitokea nyumbani kwao Wilaya ya Mpwapwa ndipo wakapata ajali,” amesema Profesa Mwamfupe. 

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Dodoma, Dk Ernest Ibenzi amesema walimpokea ofisa huyo lakini baada ya vipimo walibaini alishafariki.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa, tuliambiwa alipata ajali katika eneo la Mbande barabara ya Dodoma - Morogoro saa moja kasoro asubuhi,” amesema Dk Ibenzi.

Hata hivyo amesema hawajapokea majeruhi katika ajali hiyo.

Chanzo cha ajali bado hakijajulikana na jitihada za kupata undani wa ajali hiyo zinaendelea.

Chanzo: mwananchi.co.tz