Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Official Lyyn akiri kutoka na mastaa wawili Bongo

LYYN Df Official Lyyn

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva na muuza nyago kwenye video za muziki Bongo, Official Lyyn amekiri kutoka kimapenzi na mastaa wawili wa Bongo.

Lyyn amefunguka hayo wakati akijibu swali la mtangazaji wa kipindi cha Lavi Davi cha Wasafi FM, Diva The Bawse.

Swali La Diva: Umekuwa kwenye mahusiano na wanaume wangapi Maarufu ?

Official Lyyn: "Nimekuwa kwenye mahusiano na Wanaume wawili maarufu Diamond Platnumz na Tommy Flavour, Tommy niliachana nae sababu ya tabia tu, alirudia mara tatu.

"Mimi sio mvumilivu kwenye mapenzi, sina huo moyo wa uvumilivu, staki shida, as long as nakula, navaa , nalala, na enjoy, hujaja kwenye maisha yangu kunipa stress," alisema Lyyn

Chanzo: www.tanzaniaweb.live