Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odemba hataki kabisa kuitwa mzee

Odembaaa Odemba hataki kabisa kuitwa mzee

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miriam Odemba; ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na msanii mpya wa Bongo Fleva ambaye anasema kuwa, kwenye Sanaa yeye ni lejendari, lakini hapendi kabisa kuitwa mzee.

Odemba amejikuta akishambuliwa na kuitwa mzee baada ya kudaiwa kuwa kwenye penzi la mchongo na msanii wa Konde Gang, Ibraah ambaye wengine wanasema ni sawa na mwanawe.

Odemba mwenye umri wa miaka 39 anasema kuwa, wanaomuita mzee wamuangalie vizuri kwani bado ni mtoto mbichi kabisa.

“Wanaoniita mzee waniangalie vizuri, mimi baby girl…” Anasema Odemba kisha anaongeza; “Mimi ni staa, sijaingia kwenye muziki kwa ajili ya kutafuta kiki, mimi ni staa kitambo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live