Mlimbwende wa Kitambo Bongo Miriam Odema amefungukia madai ya kuwa na uhusiano na bwa mdogo, Ibraah kutoka Konda Gang.
Akizungumza kwenye mahojiano aliyoyafanya na wanahabari hivi karibuni, Odemba amesema, yeye na Ibrah ni washkaji na hawana uhusiano wowote wa kimapenzi hivyo yale yaliyokuwa yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa ‘biashara’.
“Ibraah ni rafiki yangu, tunasapotiana sana kwa mambo mengi. Ni mdogo wangu ambavyo ananiita mimi dada,”alisema Odemba.
Odemba ambaye kwa sasa anajiita Queen of Singeli baada ya kujiingiza kwenye muziki huo, anasema anashirikiana sana na Ibrah na Watanzania wategemee mambo makubwa kutoka kwao.