Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Odemba, Ibra mambo hadharani

IMG 20220407 WA0011 1080x640 Odemba na Ibra mambo hadharani

Thu, 7 Apr 2022 Chanzo: dar24.com

Mwanamitindo nguli kwenye tasnia ya urembo, na mtanzania mwenye makazi yake huko nchini Ufaransa Miriam Odemba, ameendelea kuonesha mahaba mitandaoni kwa msanii Ibraah kutoka Konde Music World Wide.

Akiendelea kuonesha mahaba hayo, kundi kubwa la mashabiki limepigia mstari kuwa pengine wawili hao wako kwenye uhusiano wa kimapenzi unaoelekea kutokuwa siri kutokana na namna mrembo huyo amekuwa akiweka wazi mambo kadhaa kuhusu hisia zake kwa msanii Ibraah kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii pamoja na mahojiano kadhaa aliyokwishayafanya siku za nyuma.

Mapema leo Aprili 7, 2022, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Ondemba amechapisha kipande cha wimbo wa Ibraah na kuchapisha ujumbe maalum akiuelekeza kwa msanii huyo kama sehemu ya kudhihirisha hisia zake.

“My love, kila binadamu aliyeumbwa na hisia huwa ana sehemu ya kuupumzisha moyo wake, kiukweli mimi mwili wangu unaishi Paris Ufaransa lakini moyo wangu naupumzisha Tanzania, tena nisifiche hisia zangu ni kwa Mtanzania asie na shida na mtu, ni kijana, handsome boy, mkarimu, mpole , mpambanaji na anayejali.

Hayo mengine ya hivi mara vile ni ya wananzengo, kwa hiyo nakushauri wewe msichana, wewe mwanamke na wewe mwanaume usije ukaficha hisia zako kwa kuwaogopa wajumbe wa Instagram, jali hisia zako.” Ameandika Miriam.

Ikumbukwe takribani mwezi mmoja uliopita mrembo huyo alikuja nchini Tanzania kwa ajili ya hafla yake maalum ya kusherehekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa.

Katika mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari Odemba alisema kuhusu ukaribu wake na Ibraah na kiwango cha upendo alionao kwake licha ya kutoweka uwazi ikiwa ni kweli wapo katika uhusiano wa kimapenzi au La.

Chanzo: dar24.com