Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Obama awataja Burna Boy na Ayra kwenye orodha ya ngoma zake

Burna Boy Obama And Ayrr Star 636x371 Obama awataja Burna Boy na Ayra kwenye orodha ya ngoma zake.

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Mtaafu wa Marekani, Barack Obama saa kadhaa zilizopita ameachia Orodha ya Nyimbo 41 ambazo anazisikiliza Sana katika Kipindi hiki cha kiangazi/majira ya joto.

"Kama ambavyo nimekuwa nikifanya miaka yote, hizi ni baadhi ya nyimbo ambazo nimezisikiliza kwenye majira ya joto, ni mchanganyiko wa nyimbo za zamani na mpya. Nasubiri kusikia ni wimbo gani nimeusahau," amesema Obama.

Imekuwa ni utaratibu wa Rais huyo msaafu kila mwaka Mara Mbili Anataja Orodha ya Nyimbo zake Pendwa.

Katika Orodha hiyo Wimbo wa Ayra Starr "Sability" Umetajwa. Baada ya Ayra Starr Kuona Wimbo wake katika Orodha hiyo Amefurahi sana kwani Hata Mwaka Jana Wimbo Wake "Rush" Ulitajwa na Obama.

"Rush last year , sability this year ! They will fall in line one by one"-Ayra Starr.

Mbali na "Sability" wimbo Mwingine uliotajwa Kutoka kwa Mwanamuziki wa Afrika ni "Sittin' On Top Of The World" ya Kwake Burna Boy ft 21 Savage.

Tazama Nyimbo 41 Zilizotajwa na Obama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live