Aliyekuwa rais wa awamu ya 44 wa Marekani, Barack Obama Jumanne alikuwa anasherehekea miaka 30 katika ndoa na mkewe Michelle Obama.
Rais huyo mstaafu aliachia ujumbe wenye mvuto wa aina yake kwa mkewe Michelle huku akimwambia kwamba safari yao katika ndoa kwa miaka 30 imemfunza mengi ya kujivunia na wala hawezi kujutia uamuzi huo alioufanya miongo mitatu iliyopita akiwa kijana sharobaro.
Obama alimsifia mkewe kwa kumlinganisha na kushinda kifurushi kikubwa sana siku ambacho rasmi alimvisha pete ya harusi na kulifunua shela jeupe kuona uso wake uliokuwa umeng’aa kama nyota ya alfajiri.
“Miche, Baada ya miaka 30, sijui kwa nini unaonekana sawa na sijui. Ninajua kwamba nilishinda bahati nasibu siku hiyo—kwamba singeweza kuomba mwenzi wa maisha bora zaidi. Heri ya kumbukumbu ya miaka, mpenzi!” Obama alimmiminia sifa na kumvisha koja la maua mkewe Michelle Obama.
Kwa upande wake, Michelle alimtungia ujumbe mzuri Obama huku akisema ndiye mwanaume wa kipekee ambaye anapenda na miaka 30 iliyopita alifanya uamuzi wa maana maishani mwake.
"Heri ya kumbukumbu ya miaka kwa mwanaume ninayempenda! Miaka hii 30 iliyopita imekuwa ya kusisimua, na ninashukuru kuwa na wewe kando yangu. Hapa ni kwa maisha ya pamoja. Nakupenda, @BarackObama!" Michelle aliandika.
Rais huyo wa kwanza kabisa kuwahi kutokea kuiongoza Marekani akiwa na asili ya Afrika alihudumu kama rais kwa miaka 8 ambayo ni sawa na mihula miwili katika katiba ya Amerika kutoka mwaka 2008 hadi mwaka 2016 aliporithiwa na tajiri Donald Trump kutoka mrengo wa Republican.
Obama alipata sifa tele katika uongozi wake haswa mwaka wa 2011 alipoongoza majeshi ya Markani kufanya operesheni nchini Afhanstan na kumuua adui mkubwa wa Marekani, jambazi Osama bin Laden amabye kwa zaidi ya miaka 10 alikuwa akitafutwa kwa udi na ambary na dola ya Marekani.