Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Nyumba alimozaliwa Adolf Hitler kugeuzwa kituo vya polisi

Adolf Hitler G Nyumba alimozaliwa Adolf Hitler kugeuzwa kituo vya polisi

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyumba ambayo Dikteta Maarufu Duniani, Adolf Hitler alizaliwa nchini Austria, inatarajia kugeuzwa kuwa kituo cha Polisi.

Serikali ya Austria imetangaza kuwa kituo hiko cha Polisi pia kitakuwa na kitengo cha kutolea mafunzo ya haki za binadamu.

Serikali hiyo ilifanikiwa kuchukua umiliki wa nyumba hiyo mwaka 2016 baada ya mvutano mkubwa na aliyekuwa mmiliki wake wa awali.

Ukarabati wa nyumba hiyo lenye ukubwa wa mita za mraba 799 iliyopo katika mji wa Braunau am Inn unakadiriwa kugharimu kiasi cha Pauni Milioni 17.

Kazi ya ukarabati imepangwa kuanza mwezi Oktoba na kituo hicho kinatarajia kuwa tayari mwaka 2025 na kuanza kazi rasmi mwaka 2026.

Hitler hakuwahi kukaa kwa muda mrefu sana kwenye nyumba hiyo, hata hivyo nyumba hiyo imekuwa kivutio cha watu wengi kutoka pande mbalimbali za dunia wanaoona huruma ya utawala wa Nazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live