Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota yangu ni kali kama ya Diamond-Jike Shupa

Jike Shupa Nyota yangu ni kali kama ya Diamond-Jike Shupa

Sun, 4 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo Jike Shupa amefunguka kuwa, nyota yake ni kali kama ilivyo ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Amesema ndio maana, tangu alipouza sura kwenye wimbo wa Jike Shupa wa Nuh Mziwanda aliomshirikisha Alikiba ni takribani miakia sita imepita lakini mpaka leo bado watu wanamfuatilia.

“Tangu nilipouza sura kwenye Jike Shupa na jina langu likaanzia hapo, inafika mpaka miaka sita au saba lakini bado watu wananitambua mjini,” alisema Jike Shupa.

Msanii huyo alisema, kwa sasa mbali na kuwa na umaarufu wa kuuza sura mitandaoni, anajishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo chakula na losheni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live