Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa TikTok jela miaka 6 kwa kusafirisha dawa za kulevya

Modou Adams Smuggle Nyota wa TikTok jela miaka 6 kwa kusafirisha dawa za kulevya

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota maarufu wa TikTok wa Uingereza Modou Adams (25), amekutwa na hatia ya kujaribu kusafirisha Kilo 2.9 za dawa za kulevya aina ya Cocaine kutoka Peru.

Mahakama nchini Peru imemhukumu Adams kifungo cha miaka 6 na miezi 8 na ametakiwa kulipa faini kwa makosa hayo.

Takribani wiki nne zilizopita nyota huyo aliposti picha kupitia mtandao wa Instagram akiwa kwenye maeneo ya kihistoria ya Machu Picchu kwenye milima ya Andes huko Peru.

Mnamo Septemba 30 alikamatwa na dawa hizo katika sanduku lake baada ya kusimamishwa na kukaguliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jorge Chavez.

Dawa hizo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya pauni 300,000 zilikuwa zimefichwa katika sanduku ambalo lilitakiwa kuelekea Paris na baadae kuingia London.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, Mahakama Kuu ya Peru imeposti picha mitandaoni ikimuonyesha Adams akiwa kifungoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live