Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa Black Panther kuwanoa Bongo muvi

8afb092f035cba45a8073ede14c00d46 Nyota wa Black Panther kuwanoa Bongo muvi

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MUIGIZAJI aliyetia nakshi kubwa katika sinema ya Black Panther, Connie Temweka Gabisile Chiume amewasili nchini kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa bodi ya filamu nchini ikishirikiana na Taasisi ya Re focus Africa .

Muigizaji huyo raia wa Afrika kusini mwenye asili ya Malawi anatarajiw akuwanoa waigizaji wa Bongo Movie.

Muigizaji huyo ambaye aliwasili nchini juzi pia ameshiriki katika sinema za Black Is King na Blessers na kushiriki katika tamthilia za Zone 14 na Rhythm City.

Connie anayefanya kazi zake Marekani alipokewa nchini na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Filamu, katika Bodi ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa na wadau wengine wa filamu.

Akizungumza wakati wa ujio wa nyota huyo kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere, Ndumukwa alisema ni tukio la furaha kwa kuwa nyota mwenye jina kubwa Marekani anakuja kunoa wasanii wa Bongo muvi.

“Miongoni mwa faida zitakazopatikana kutokana na ujio wa msanii huyu ni kuimarisha soko la filamu za hapa nchini kimataifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kupata elimu ya uigizaji wa kimataifa na kuongeza elimu kuboresha kipaji,” alisema Ndumukwa.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya ReFocus Africa, Kanali Mstaafu Iddi Kipingu alishauri wadau wa Bongo muvi kufika kwenye mafunzo hayo yatakayotolewa na msanii huyo ambaye ni mwalimu mzoefu wa kimataifa katika masuala ya uigizaji.

“Huyu ni staa wa uigizaji pale Marekani ana heshima kubwa kupitia sanaa ya uigizaji na ametunukiwa tuzo nyingi tu za kimataifa hivyo ni vyema wadau wakajitokeza kupata mafunzo hayo ambayo yataambatana na vyeti kwa wahitimu,” alisema Kipingu.

Mkongwe wa filamu za kuigiza Sabrina Mjata ‘Zawadi’ aliwashauri wasanii wenzake kuacha kukaa majumbani kwa kuona wanajua kila kitu kwenye uigizaji bali wajitokeza kwenye mafunzo hayo kutoka kwa gwiji wa ufundishaji wa kimataifa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz