Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoshi amkumbuka Magufuli alivyokuwa mkweli

2b256eeba86c7f9e4e5c50760221cac9.jpeg Nyoshi amkumbuka Magufuli alivyokuwa mkweli

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa dansi, Nyoshi El Sadaat amesema hatamsahau Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwani alikuwa kiongozi mkweli na amefanyia kazi mengi aliyowaahidi wasanii.

Akizungumza Dar es Salaam jana, msanii huyo alisema Magufuli alikuwa tofauti na viongozi wengine ndani ya miaka mitano aliyotumikia Tanzania kwani amefanya mambo makubwa ya maendeleo na kuonesha dhahiri alikuwa mtu wa vitendo.

“Magufuli alikuwa akipenda maendeleo ya nchi yake, tumetembea nchi nyingi na kushuhudia marais wanaahidi kufanya mambo fulani lakini baadaye hawatekelezi kwa haraka kama alivyofanya kiongozi huyo,” alisema.

El Sadaat alisema ndani ya muda mfupi nchi inaonekana kama Ulaya jambo linaloonesha kuwa hakuwa mtu wa maneno tu.

Alisema kwa kuwa hayupo tena, watu wamuunge mkono Rais wa Sita wa Awamu ya Tano, Samia Suluhu Hassan ili akafaye kazi iliyoachwa na Magufuli.

“Tumuunge mkono Mama Samia ili apate nguvu ya kuongoza nchi, tunachomuomba kwake ashirikishe watu ili wajenge nchi kwa amani na sisi wanamuziki tunamuombea,” alisema.

Alisema ana imani atawakumbuka wasanii na makundi mbalimbali na kuwaunga mkono.

Chanzo: www.habarileo.co.tz